Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila Odinga ataka Interpol kuongoza uchunguzi wa kifo cha mshukiwa wa ICC Kenya
Kimataifa

Raila Odinga ataka Interpol kuongoza uchunguzi wa kifo cha mshukiwa wa ICC Kenya

Raila Odinga
Spread the love

 

KIONGOZI wa Azimio Raila Odinga amewataka polisi wa Kimataifa wa Interpol kuanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mshukiwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), wakili Paul Gicheru.

Katika taarifa iliotolewa na msemaji wa Raila Prof Makau Mutua mnamo Jumatano, Septemba 28, Raila alitaja kifo hicho kuwa cha kushangaza na kisichoelezeka.

“Mfano wa vifo vya ajabu na visivyoelezeka, vingine vikiwa vya kutisha na vibaya, ni vya kutatanisha sana.

Amesema kwamba ili kuzuia mauaji hayo kuzimwa, amewataka maafisa wa Interpol kuongoza Uchunguzi huo, ilisema Taarifa hiyo.

Raila alieleza kuwa kifo cha Gicheru kilikuwa na athari za kimataifa kwani ICC ilimweka kizuizini wakati wa kifo chake.

Alisema kuwa kwasababu ya kuwa mwanachama wa Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague, Kenya haikuwa na chaguo ila kuruhusu uchunguzi.

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliifariji familia ya Gicheru na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu ugonjwa wa mwana wao.

Gicheru alikuwa ameshtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa kuingilia mashahidi kuhusiana na kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08, ambapo alikana mashtaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!