Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mwalimu Benki yazindua “Bando la Mwalimu”, Serikali yatoa neno
Elimu

Mwalimu Benki yazindua “Bando la Mwalimu”, Serikali yatoa neno

Heri James, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
Spread the love

BENKI ya Mwalimu imezindua Bando la Mwalimu kupitia kampeni yake ya ‘Asante Mwalimu’ yenye lengo la kurudisha shukrani kwa mwalimu, ambapo Serikali imeahidi kuendelea kuthamini mchango wa walimu na kuwajali kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu kuanzia majengo, vitendeakazi ikiwa pamoja na kuwalipa stahiki zao zote muhimu. Anaripoti Mary Victor, Dar es Salaam … (endelea).

Kampeni hiyo ilezinduliwa jana Septemba 28, 2022 katika tawi letu la Mlimani Tower jijii Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James ambapo alisema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa walimu ikiwa pamoja na kuwajali.

Alisema katika maboresho hayo Serikali itahakikisha walimu wanalipwa malimbikizo na stahili zao, wanakwenda likizo kwa wakati na kupanda madaraja kwa wenye sifa na vigezo stahili.

Mkuu wa Wilaya huyo aliipongeza Banki ya Mwalimu kwa hatua iliyoichukua kuwabeba walimu kuanzia wakiwa chuo moaka wanapoingia kazini kwani hiyo ni hatua kubwa sana na msaada mkubwa kwa serikali katika kumthamini mwalimu na taaluma yake.

“Ninyi Mwalimu benki nawapongeza kwa kuwa mnajali sekta ya elimu. Nimeona bando lenu lina mkusanyiko wa huduma muhimu kwa mwalimu tangu akiwa chuo, serikali inajivunia sana uwepo wa Mwalimu Benki,” alisema James na kuongeza.

“Mwalimu ni mtu muhimu hakuna namna tunaweza fanikiwa bila mwalimu hivyo utulivu wa mwalimu unabebwa na Mwalimu benki kwa kupata huduma bora za kibenki kwa gharama nafuu sana.”

Dhumuni la kampeni hii inayoelekea maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani ni kuunga mkono juhudi kubwa za serikali katika kuhakikisha walimu wanakua na mazingira bora kwenye utoaji huduma kwa jamii na hata baada ya utumishi wao, vile vile kampeni hii imelenga kurudisha shukrani zetu za dhati kwa walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuelimisha na kukuza taifa kwa ujumla.

Kupitia kampeni hii ya “Asante Mwalimu, Mwalimu Benki itakuwa na “Bando la Mwalimu” ambalo ni mkusanyiko wa bidhaa mbalimbali zinazomlenga mwalimu moja kwa moja zikiwa na lengo la kumpatia suluhisho la kifedha na zaidi kumlinda Mwalimu na athari kubwa za mikopo umiza ambayo imeendelea kuwa kilio kikubwa kwa walimu wetu.

Bidhaa zipatikanazo kwenye “Bando la Mwalimu” ni Career Account ambayo ni maalum kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu na vyuo vingine mbalimbali, Mwalimu Jikimu, maalum kwa walimu wanaonza ajira unaowawezesha kukidhi mahitaji muhimu ya awali, Ada chap chap huu ni mkopo wa haraka kwa ajili ya ada ya shule kwa walimu wanaotaka kujiendeleza kielimu, Salary Advance, huu ni mkopo waharaka kwa ajili ya kukidhi dharura mbalimbali ambapo mwalimu ataupata.

Mabando mengine ni kama Mchongo Fasta, huu pia ni mkopo wa dharura wenye kiwango kikubwa zaidi ya malipo ya awali ya mshahara, Mwalimu Personal Loan, huu ni mkopo binafsi na mahsusi kwa ajili ya Mwalimu, Mlinde Mstaafu, huu ni mkopo maalumu wenye riba nafuu kwa wastaafu wanaosubiri kulipwa mafao na Wastaafu Loan, mkopo maalum kwa ajili ya Wastaafu wenye riba nafuu kabisa, unaomuwezesha mstaafu kuendelea kufanya maendeleo ya kiuchumi na mipango mingine mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!