Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Haya hapa mambo matatu waliyoteta Rais Samia, Dk. Ruto
Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa mambo matatu waliyoteta Rais Samia, Dk. Ruto

Spread the love

SAA chache kabla ya kuapishwa kuwa Rais wa tano wa Kenya, Dk. William Ruto ameteta na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili nchini humo mapema leo kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Rais Samia Suluhu Hassan na Dk. William Ruto

Leo tarehe 13 Septemba, 2022 Dk. Ruto katika ukurasa wake wa Twitter, ameweka picha mbalimbali akiwa na Rais Samia na kuandika kuwa Serikali yake itashirikiana na Tanzania katika biashara, kilimo, usalama na maeneo mengine.

Ruto ameandika, “Tutapanua ushirikiano wetu na Tanzania katika biashara, kilimo, usalama miongoni mwa maeneo mengine yenye maslahi, mbali na kufanya kazi pamoja kwa nia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa manufaa yetu sote.”

Hata hivyo, mbali na Rais Samia, Ruto amekutana na kuzungumza na viongozi wa mataifa mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake zinazofanyika katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!