Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Yanga yatangaza viingilio siku ya mwananchi, tiketi VVIP zamalizika ndani ya saa 3
HabariMichezo

Yanga yatangaza viingilio siku ya mwananchi, tiketi VVIP zamalizika ndani ya saa 3

Spread the love

 

klabu ya soka ya Yanga yenye makazi yake mitaa ya Jagwani na Twiga jijini Dar es salaam imetangaza rasmi viingilio vyote vitakavyotumika katika  siku ya wiki ya mwananchi itakayofanyika, huku tiketi za VVIP[ zikimaliza muda mfupi mara baada ya kuanza kuuzwa. Anaripoti Damas Ndelema….(endelea)

Tamsha hilo lenye hamsha hamsha ndani yake, litafanyika tarehe 6 Agosti 2022, kuanzia majira ya asubuhi kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Tiketi hizo zilitangazwa kuanza kuuzwa rasmi kwenye tukio la ufunguzi wa wiki ya wananchi, lilifanyika hii leo tarehe 1 Agosti 2022, kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam kwa kuatajwa vituo zitakazopatikana sambamba na bei zake.

Kuelekea tamasha hilo tiketi ya bei ya chini itauzwa kwa shilingi 10,000, VIP C itakuwa shilingi 20,000, VIP B shilingi 30,000, huku VIP A ikiwa ni shilingi 150,000 ambapo shabiki atapewa jezi moja ya nyumbani bure usafiri wa kwenda na kurudi kutokea Serena Hotel.

Tiketi nyingine zilizotangazwa kuuzwa ni VVIP ambapo zilikuwa zinauzwa kwa shilingi 300,000, lakini tayari zimemalizika ndani ya muda mchache.

Taarifa za kumalizika kwa tiketi hizo, zimetolewa kupitia kurasa rasmi ya klabu hiyo kupitia mitandao mbaalimbali ya kijamii.

Kuelekea kwenye tukio hilo, uongzoi wa klabu hiyo kupitia kamati maalumu ya iliyoundwa kwa ajili ya tukio hilo, uliweka wazi kuwa kikosi chao kitashuka dimbani siku hiyo dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipres FC.

Pia kamati hiyo imetangaza kauli mbiu itakayotumika ktika kunogesha shughuli hiyo inayoitwa “Byuti Byuti” ambayo wameitohoa kutoka kwenuye neon la kingereza “Beuty beuty” lenye maana ya zuri zuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!