August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simanzi ajali ikiua watoto wa wafanyabiashara maarufu Arusha

Spread the love

 

VIJANA wawili Estomi Temu na Nice Mawala wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 24, wamefariki dunia kwa ajali ya gari jijini Arusha usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 31 Julai, 2022. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) … (endelea).

Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo imetokea majira ya saa 7 usiku katika eneo la Kwamrefu ikihusisha gari aina ya Range Rover lenye namba za usajili T 313 ANM.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Justine Masejo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa uchunguzi unaendelea kujua chanzo chake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema vijana hao ambao wanaodaiwa kuwa ni wachumba na watoto wa matajiri wakubwa jijini humo, walipata majeraha makubwa yaliyosababisha kupoteza maisha.

Miili ya vijana hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

error: Content is protected !!