August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

M-Bet yaijaza mabilioni Simba, waipiku Yanga

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara, imesaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya kubashiri ya M-Bet kama mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwa timu kubwa ya wanaume  mkataba huo wenye thamani ya billioni 26.1. Anaripoti Damas Ndelema… (endelea)

Mkataba huo umesainiwa  leo Agosti Mosi mwaka huu, ambapo umeifanya klabu hiyo kuwa ndio yenye thamani kubwa katika klabu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu kwa msimu ujao.

Kwenye mkataba huo katika kipindi cha mwaka wa kwanza, Simba kiasi cha shilingi 4.6470, kwenye mwaka wa pili watapokea kiasi cha shilingi bilioni 4.925.

Kiasi hicho cha fedha kitaendelea kuongezeka kwenye mwaka wa tatu Siba itapewa kiasi cha  shilingi bilioni 5.205, na mwaka wa nne watapewa shilingi bilioni 5.514 na mwaka wa tano ambao ndio wa mwisho wa mkataba watapewa shilingi bilioni 5.853.

Mkataba huo ni mkubwa kuliko ule waliosaini wapinzani wao klabu ya Yanga, siku chache zilizopita na kampuni ya kubashiri ya Sports Pesa wenye thamani ya shilingi bilioni 12 kwa kupindi cha miaka mitatu.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoudhuliwa na waandishi wa habari, Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa mchakato wa kutafuta mdhamini mkuu ulianza toka mwaka jana mwezi wa kumi na moja na makapuni yalikua mengi lakini M-Bet ndio waliokizi mahitaji ya Simba, pia mkataba huo ni kwa utahusisha timu ya wanaume pekee na sio za vijana na wanawake na kama akitokea mdhamini basi watamkaribisha mezani kwa ajili ya mazungumzo.

“Mkataba huu ni kwa ajili ya timu kubwa ya wanaume hauhusiani na timu za vijana au timu ya wanawake (Simba Queen) kama tukitaka kutafuta tena mdhamini wa Simba queens na timu za vijana  basi tutakaa tena mezani kwaajili ya mazungumzo” Alisema mtendaji huyo

Kwa upande wa wadhamini hao ambao waliwakilishwa na Allan Mushi amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya shilling bilioni 26.1 kwa mda wa miaka mitano na wameungana na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa nchini Tanzania na inawakilisha vizuri nchi kuimataifa.

“Sisi kama M-Bet tuna amini kuwa tukishirikiana vizuri na Simba tutajitangaza ndani na nje ya Tanzanania maana Simba ni timu kubwa” Alisema Mushi

Pia mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi  ya Simba Abdallah amesema Simba inawashukuru wadhamini waliopita na sasa wapo na wadhamini wa wapya pia milango ipo wazi kwa makampuni maana bado kuna Simba queens na timu za vijana sababu Simba ni klabu ya watu wako tayari kufanya kazi na watu wote , pia akiwashukuru M-Bet na kuwaahidi watakipata walichokitaka maana wametoa pesa nyingi

“M-Bet mlichokitaka mtakipata , pesa ni nyingi hizi tumieni hii nafasi ya mtaji wa mashabiki wetu kutanua biashara yenu” Alisema M/kiti huyo wa bodi

Aidha pia mkurugenzi wa michezo ya kubahatisha amepongzea mkataba huo na kuisisitiza M-Bet kufanya kazi kwa makini ili izidi kupata mikataba mingi na kuendelea kuiheshimisha michezo ya kubahatisha kwa ujumla.

Huu ni mkataba wa kwanza wa Simba wa udhamini mkuu wa klabu aambao wamesaini, toka walipoingia kwenye mfumo wa mabadiliko ya uwendeshaji wa timu katika kipindi cha miaka mnne iliyopita.

error: Content is protected !!