Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jafo awafunda wanahabari, awakumbuka utunzaji mazingira
Habari Mchanganyiko

Jafo awafunda wanahabari, awakumbuka utunzaji mazingira

Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo amewataka wanahabari nchini kujenga tabia ya upendo na kujaliana wakati wote wa shida na raha.

Pia amesema uandishi wa habari ni sehemu ya huduma ya utoaji elimu kwa jamii hivyo ni vyema wanatasnia hao wakajenga hulka ya kushirikiana kwa upendo badala ya kujengeana fitina na majungu yasiyo kuwa na sababu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Amesema kuwa wanahabari nchini ni wadau muhimu katika kutoa elimu kwa jamii hususani elimu juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Jafo ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Julai 2022 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma wakati wa chakula cha pamoja baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi katika soko la Bonanza lililopo jijini Dodoma.

Jaffo amesema wanahabari wamekuwa nguzo kubwa katika kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni pamoja kuelezea umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Aidha Jafo ameeleza kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni sehemu ya ibada kwani mazingira yanaweza kufanya mabadiliko ya tabia ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!