August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafugaji waiangukia Serikali uhaba wa maofisa mifugo

Spread the love

SERIKALI imeombwa kuhakikisha inapeleka wataalamu wa mifugo kwa wafugaji ili kuweza kufanya ufugaji wenye tija. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 30 Julai mwaka 2022 na Amoss Mwanyovellah ambaye ni moja wa wafugaji alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa kisasa.

Mfugaji huyo amesema pamoja na kuwepo na changamoto mbalimbali lakini bado kuna tatizo la matibabu ya mifugo bado ni gharama kubwa ikiwamo kuwapatia mifugo yao chanjo.

Akizungumzia upatikanaji wa maziwa amesema kuwa kutokana na matunzo bora ya ng’ombe wake anauhakika wa kupata lita za maziwa 30 kwa ng’ombe mmoja kwa siku jambo ambalo amesema anajipatia kipato cha kutosha kupitia mifugo hiyo.

Mfugaji huyo amesema ufugaji wa mifugo ya kisasa kama vile ng’ombe wanahitaji uangalizi makubwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia matibabu ya mara kwa mara.

Aidha, Mwanyovellah ameeleza pamoja na kuwepo kwa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa bado kuna changamoto kubwa ya matibabu kutokakana na kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa wataalamu wa matibabu kwa mifugo.

“Suala la matibabu kwa mifugo ni changamoto kuwa kwani unapokuwa na mifugo au unapokuwa na ng’ombe wenye thamani ya milioni tano na unahitaji mtaalamu wa tiba ya mifugo anaweza kuja mtaalamu na kujifanya kuwa mfugo una ugonjwa fulani kumbe siyo sawa.

“Kutokana na hali hiyo serikali naiomba isambaze zaidi wataalamu wa mifugo ili kutambua makundi ya wafugaji wa kisasa na kienyeji,” ameeleza mfugaji Huyo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Dodoma halisi, Anthony Msanga amewataka wafugaji kuhakikisha wanafuga ufugaji wa kibiashara na wenye tija badala ya kufuga kwa mazoea.

Msanga amesema kuwa ufugaji wa kisasa utasaidia kuongezeka kwa upatikanaji wa maziwa jambo ambalo litasaidia mfugaji kujiongezea kipato lakini pia kuondoa udumavu wa watoto pamoja na watu wazima kwa kukosa virutubisho vinavyotokana na maziwa.

“Kwa mujibu wa maelezo ya afya juu ya utumiaji wa maziwa ni kwamba kila mtanzania anatakiwa kutumia lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini watanzania wengi wanatumia kiwango cha chini cha maziwa

“Watanzania kwa sasa wanatumia kiwango kidogo cha maziwa kati ya lita 60-64 kwa mwaka badala ya lita 200 kwa mwaka,” amesema Msanga.

error: Content is protected !!