August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiboko ‘babu’ aliyeua watu 8, auawa

Spread the love

KIBOKO dume ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisumbua wananchi wa kata ya Mabilioni wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro na kukwamisha shughuli za maendeleo kama kilimo, ufugaji na uchotaji wa maji katika Mto Pangani, ameuawa kwa kupigwa risasi katika msako ulioongozwa na vikosi kutoka TAWA. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogoro akizungumza baada ya kiboko Babu kuuawa.

Kiboko huyo aliyepewa jina la Babu ambaye ameua watu zaidi ya sita, ng’ombe 8, punda na mbuzi tangu mwaka 2017 alikuwa akihusishwa na imani za kishirikina kwani jitihada mbalimbali za kumdhibiti hazikufanikiwa katika kipindi chote

Tarehe 17 Juni 2022 kiboko huyo alimuua kwa kumshambulia mwanaume mmoja aliyekuwa anakwenda shambani kumwagilia ndipo Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo alipoagiza kuhakikisha kila mbinu zinatumika kumuua kiboko huyo ili wananchi warudi kufanya shughuli za maendeleo kwa amani.

Baada ya kuanza msako kiboko huyo aliuawa tarehe 28 Julai 2022 saa 11 alfajiri baada ya kuweka mtego na kupigwa risasi ya kichwa na Mzee Ally Miraji Sengela (hunter) aliyesaidiwa na Mzee Fue Omary Ngerwa (Mvuvi na Mweka Mtego) kwa kushirikiana na wahifadhi wa TAWA.

error: Content is protected !!