Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Balozi nne zakiuka taratibu, zalipa milioni 239
Tangulizi

Balozi nne zakiuka taratibu, zalipa milioni 239

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere amebaini balozi nne zilifanya malipo yenye thamani ya Sh.239.56 milioni zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na bila ushahidi wa kibali cha kuhamisha fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika ripoti yake inayoishia tarehe 30 Juni 2021 ambayo jana Jumanne 12 Aprili 2022 ameiwasilisha bungeni jijini Dodoma, CAG Kichere amesema “malipo kinyume na bajeti huathiri utekelezaji wa shughuli zilizopangwa, na hivyo kupelekea kutofikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.”

CAG amesema, “ninapendekeza menejimenti ya balozi husika kuhakikisha kuwa matumizi yote yanazingatia bajeti iliyoidhinishwa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Bajeti.”

Amezitaja balozi hizo na kiwango cha malipo ilichokifanya ni, Ubalozi wa Tananzania mjini Doha Sh.74.4 milioni, Ubalozi wa Tanzania- The Hugue Sh.45.4 milioni, Ubalozi wa Tanzania- Brussels Sh.5.3 milioni na Ubalozi wa Tanzania- Moroni Sh.114.3 milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!