MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere amebaini balozi nne zilifanya malipo yenye thamani ya Sh.239.56 milioni zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na bila ushahidi wa kibali cha kuhamisha fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Katika ripoti yake inayoishia tarehe 30 Juni 2021 ambayo jana Jumanne 12 Aprili 2022 ameiwasilisha bungeni jijini Dodoma, CAG Kichere amesema “malipo kinyume na bajeti huathiri utekelezaji wa shughuli zilizopangwa, na hivyo kupelekea kutofikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.”
CAG amesema, “ninapendekeza menejimenti ya balozi husika kuhakikisha kuwa matumizi yote yanazingatia bajeti iliyoidhinishwa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Bajeti.”
Amezitaja balozi hizo na kiwango cha malipo ilichokifanya ni, Ubalozi wa Tananzania mjini Doha Sh.74.4 milioni, Ubalozi wa Tanzania- The Hugue Sh.45.4 milioni, Ubalozi wa Tanzania- Brussels Sh.5.3 milioni na Ubalozi wa Tanzania- Moroni Sh.114.3 milioni.
Leave a comment