Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wananchi 10,000 kufaidika na Kituo cha Afya Sangambi
Afya

Wananchi 10,000 kufaidika na Kituo cha Afya Sangambi

Spread the love

ZAIDI ya wananchi 10,000 kutoka katika Kata ya Sangambi, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wanatarajiwa kupata unafuu wa matibabu baada ya Kituo cha Afya cha Sangambi kuanza kutoa huduma miezi michache ijayo baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Unafuu huo unatokana na ukweli kwamba katika kata hiyo hakuna kituo cha afya na wakihitaji huduma za ngazi hiyo wanalazimika kwenda Chalangwa ambako kuna umbali wa kilomita 19 au hospitali ya wilaya ambayo pia iko umbali wa kilomita zaidi ya 23.

Mmoja wa wananchi hao Happiness Obadia ambaye ni mkazi wa Sangambi, amesema sasa hivi wanapata huduma za matibabu makubwa katika hospitali ya wilaya ya Chunya yenye umbali wa kilomita 23 kutoka Sangambi.

“Tunapata changamoto kubwa kwa sababu sio wananchi wote wenye uwezo wa kusafiri umbali huo kuwapeleka wagonjwa Chunya. Inatokea wakati mwingine, mtu amezidiwa ghafla hadi ufanye mawasiliano wilayani na gari la wagonjwa, mgonjwa anakuwa katika hali mbaya zaidi.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na wazo wa kujenga vituo vya afya katika vijiji mbalimbali kikiwemo cha Sangambi, vitasaidia kurahisisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa ukaribu zaidi,” amesema Happyness.

Happyness amesema eneo kulikojengwa kituo cha afya kunapatikana wananchi mbalimbali wakiwemo wafugaji wanaopenda kukaa vijijini kutokana na asili ya shughuli zao, hivyo kuwepo kwa huduma hiyo, kutasaidia kuwapunguzia umbali wa kwenda wilayani kufuata matibabu.

Naye Joseph Kihwele amesema kituo hicho, kikikamilika watapata huduma kwa ukaribu tofauti na hivi sasa wanazipata mbalimbali, hali inayosababisha kutembea umbali mrefu wakiwa na wagonjwa kwenda katika vituo vya afya vya jirani au hospitali ya wilaya.

“Miongoni mwa kituo cha afya cha jirani kipo kata ya Chalangwa ambapo kuna kilomita 19 kutoka hapa.Utaona ni umbali kiasi gani wananchi wa Sangambi wanatembea kufuata huduma za ngazi ya kituo cha afya, tunashukuru uwepo wa kituo hiki cha kisasa,” amesema Kihwele.

Kihwele amesema mtoto wake wa mwisho ana miaka miwili sasa, anabainisha kuwa endapo kituo hicho cha afya kingekuwapo wakati huo, basi asingelazimika kutumia gharama kubwa ya kumsafirisha mkewe badala yake fedha zilizobaki zingetumika kununua vifaa vingine kwa ajili ya mkewe na mtoto.

“Sasa wananchi wa Sangambi wakiwa wanafikiria kupata au kuongeza watoto hawatakuwa na sababu ya kuwaza umbali wa kituo kwa sababu kipo karibu na huduma bora zitapatikana hapa. Tuna wahamasisha wake zetu wapunguze uzazi wa mpango ili kituo hiki kipate wateja wa kutosha,” amesema Kihwele.

Aidha, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Sangambi, Dk. Kanuti Matamwa amesema mradi huo ulianza Oktoba mwaka jana na kituo hicho chenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni kikianza kutoa huduma, kitapunguza adha ya wananchi wa eneo kwenye Chunya mjini kutafuta huduma za ngazi juu.

“Kituo hiki kinajumuisha jengo la wagonjwa wa nje, upasuaji, wodi ya wazazi kwa ajili ya kina mama waliojifungua na wanaosubiri kujifungua. Tuna jengo la maabara litakalotusaidia kwa ajili ya uchunguzi wa wagonjwa,” amesema Matamwa.

Mbali na hilo, Matamwa amesema kituo hicho cha afya cha kisasa kitakuwa na jengo la kuhifadhia maiti.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya kwa wananchi wa Sangambi na kuongeza kuwa mkuu huyo wa nchi ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake amefanya makubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!