Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia ataka mfuko wa pembejeo kukabili mfumuko wa bei
Habari Mchanganyiko

Rais Samia ataka mfuko wa pembejeo kukabili mfumuko wa bei

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Kilimo ianzishe mfuko wa pembejeo na wa maendeleo ya kilimo, kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya mfumuko wa bei za pembejeo kwa wakulima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 4 Aprili 2022, akizindua ugawaji vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo, jijini Dodoma.

“Nitoe agizo muanzishe mifuko ya mzunguko, ambao mnaona utakuwa wa pembejeo na wa pili wa maendeleo ya kilimo. Madhumuni tunapoenda kupata shida ya pembejeo zinapopanda bei, mfuko ushushe presha ya bei kwa wakulima. Wakulima wetu wasiende kupata kadhia ya kulipa pesa nyingi kupata pembejeo,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema atazungumza na uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili kuangalia namba ya kupata fedha za kuendesha mifuko hiyo.

Pia ameagiza jumuiya za watu wanaofanya kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia mabwawa ya Serikali, waanze kutozwa fedha kwa ajili ya kutunisha mifuko hiyo.

Rais Samia ameiagiza Wizara ya Kilimo, ifumue muundo wa Tume ya Umwagiliaji, ili kuanzisha ofisi za umwagiliaji ngazi ya wilaya kwa ajili ya kufikisha huduma karibu na wananchi.

Rais Samia ametoa maagizo hayo baada ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kumuomba atoe fedha kiasi cha Sh. 150 bilioni, kwa ajili ya kutoa ruzuku za pembejeo kwa wakulima, katika kipindi hiki ambacho kuna mfumuko wa bei ya bidhaa hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewaomba wabunge waibebe sekta ya kilimo bungeni, ikiwemo kwa kupitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo.

“Wabunge mko hapa, mmesikia mipango ya wizara, Serikali imeongeza bajeti… nawaombeni sana tubebeni sekta ya kilimo, sekta nyingine zinakwenda vizuri. Kwenye kilimo pitisheni kwa kauli moja tuweze kutekeleza,” amesema Rais Samia.

Pia, Rais Samia ameagiza eneo litakalobaki kwenye ujenzi wa Bwawa la Ufuaji Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, kwenye Mto Rufiji, litumike kwa ajili ya shughuli za kilimo.

“Wizara ya Fedha na Wizara ya Ardhi, mligawe litakwenda kwa ajili ya mazao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!