Thursday , 2 May 2024
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ametaja mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika sekta ya kilimo baada ya Serikali kuweka mikakati mbalimbali na kusema sekta hiyo sasa inaelekea kuwa uti wa mgongo wa uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ameyasema hayo jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022 wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ughani wa kilimo nchini.

Amesema ni dhahiri sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili mkuu wa kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

Amesema kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 4.9 na kuchangia asilimia 26.9 kwenye pato la taifa na kutoa ajira asilimia 61 kwa watanzania huku ikichangia asilimia 65 kwa malighafi za viwanda.

“Kwa takwimu hizo imetufanya Tanzania tujitosheleze kwa chakula asilimia 100.

Amesema pamoja na takwimu hizo bado ukuaji wa sekta ya kilimo ni mdogo na kwamba jitihada zikiongezwa zaidi itafikia ikawa ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania “na tunaelekea huko.”

Amesema licha ya kuwa na hekta 44 milioni za adrhi inayofaa na hekta 29.4 milioni ya ardhi ya kilimo cha umwagiliaji maji lakini ni asilimia ndogo ya eneo hilo inatumika.

Amesema ili kufikia azma hiyo, Serikali imeweka malengo kuongeza kasi ukuaji wa kilimo kutoka asilimia 5 hadi 5.7 “lakini waziri amesema lengo hili ni dogo sana tunaweza kwenda kufika asilimia 10 ifikapo 2025.”

Mkuu huyo wa nchi ametaja malengo mengine ni kuongeza mazao yanayouzwa nje kutoka Dola bilioni 1.2 hadi Dola bilioni 5, “ kama tutafuata mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo tunaweza kuvuka lengo hili.”

Malengo mengine kuongeza mashamba makubwa kutoka 110 hadi 1000, kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 665,000 hadi hekta milioni 1.2.

“Kwa malengo wizraa iliyojiwekea yakuongeza kilimo cha umwagiliaji kutoka asilimia 10 hadi asilimia 50 tunakwenda kuweka hekari milioni 18 kwenye umwagiliani.” amesema.

Amesema katika kuahakikisha malengo hayo yanatamia Serikali imeweka jitihada katika utafitikwa kuongeza bajeti kutoka Sh 7.35 hadi Sh 11 bilioni.

amesema wamefanya hayo kwasababu “kilimo kinaweza kuivusha nchi na nimefanya kazi ya kilimo kama miaka tisa nikifanya kwenye mifugo na mazao.”

Ameongeza pia bajeti ya huduma za ughani “hiki kilikuwa kilio kikubwa” imeongezeka kutoka Sh 17.7 bilioni hadi Sh 51.45 bilioni.

Vilevile Serikali imeongoza uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora kutoka Sh 5.4 hadi Sh 10 .5 Bilioni na kuzipa fedha Wakala wa Chakula wa Taifa na Bodi ya Mazao Mchanganyiko Sh 129 bilioni kwaajili yakununua na kuhifadhi mazao ya wakulima.

Ameongeza Serikali imekufungua masoko mapya ya mazao ikiwemo parachichi huko Uchina na Afrika Kusini, kupata maghala ya kukodi nje ya nchi tani 5000 Sudani Kusini na tani 2000 Lubumbashi nchini DRC na kwamba jitahada zingine zinaendelea kupata maghala China, Vietnam na Falme za Umoja wa Kiarabu.

“Tunafanya jitihada zote hizi ili wakulima wetu waweze kupata thamani ya jasho wanalolitoa, wale watu wa katikati wakwenda kununua mazao kwa bei ya chini wao wakauze bei ya juu hapana,” amesisitiza.

Kuhusu upotevu wa mazao baada ya uvunaji Rais Samia amesema wameelekeza kuanza kujenga maghala vijijini ambako ndiko wakulima walipo.

Takwimu zinaonyesha asilimia 30 ya mzao yanayovunwa hupotea kutokana na kutokuwa na njia bora za uhifadhi.

Amesema katika hatua nyingine wameweza kufanikisha upatikanaji wa idhibati ya ubora kwaajili ya maabara yenye viwango vya kimataifa ya mamlaka ya mimea na viuatilifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!