Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maofisa Ughani kumilikishwa pikipiki baada ya miaka miwili
Habari Mchanganyiko

Maofisa Ughani kumilikishwa pikipiki baada ya miaka miwili

Spread the love

MAOFISA Ughani nchini watamilikishwa pikipiki zinazotolewa na Serikali baada ya kuzitumia kwa miaka miwili katika kutoa huduma kwa wakulima. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022 kuridhia ombi lilotolewa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Awali Bashe alisema Serikali haiwezi kushindwa kununua pikipiki hizo kila baada ya miaka miwili hivyo ni vyema wakamilikishwa ili zinunuliwezingine.

Serikali imegawa jumla pikipiki 7000 kwa maofisa ughani ambapo leo Rais Samia amegawa pikipiki 6,700 na zingine 300 zilishatolewa.

Hata hivyo Rais Samia amesema pikipiki hizo zitamilikishwa tu kwa wale ambao wataonekana wametekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Haitakuwa blanked kwamba tutawamilikisha, hapana. Tutapima kwa kazi mnazofanya, na tunaamni kwa kipindi hicho thamani ya kazi yenu itakuwa imezidi hiyo ya pikipiki” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itawapa hari ya kufanya kazi na kuzitunza pikipiki hizo wakijua baada ya hapo watazimiliki wao.

Mbali na pikipiki pia Rais Samia amesema Serikali itagawa vipima udongo kwa halmashauri 143, kutoa simu janja pamoja na visanduku 3300 kwa maafisa ughani.

Ametumia fursa hiyokuwataka maofisa ughani kutumia vitendeakazi hivyokama ilivyokusudiwa kwa manufaa ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!