Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi
Habari Mchanganyiko

Kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi

Spread the love

 

Rais Samia Suluhu Hassan, ametaja mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika sekta ya kilimo baada ya Serikali kuweka mikakati mbalimbali na kusema sekta hiyo sasa inaelekea kuwa uti wa mgongo wa uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ameyasema hayo jijini Dodoma leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022 wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ughani wa kilimo nchini.

Amesema ni dhahiri sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili mkuu wa kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

Amesema kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 4.9 na kuchangia asilimia 26.9 kwenye pato la taifa na kutoa ajira asilimia 61 kwa watanzania huku ikichangia asilimia 65 kwa malighafi za viwanda.
“Kwa takwimu hizo imetufanya Tanzania tujitosheleze kwa chakula asilimia 100.

Amesema pamoja na takwimu hizo bado ukuaji wa sekta ya kilimo ni mdogo na kwamba jitihada zikiongezwa zaidi itafikia ikawa ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania “na tunaelekea huko.”

Amesema licha ya kuwa na hekta 44 milioni za adrhi inayofaa na hekta 29.4 milioni ya ardhi ya kilimo cha umwagiliaji maji lakini ni asilimia ndogo ya eneo hilo inatumika.

Amesema ili kufikia azma hiyo, Serikali imeweka malengo kuongeza kasi ukuaji wa kilimo kutoka asilimia 5 hadi 5.7 “lakini waziri amesema lengo hili ni dogo sana tunaweza kwenda kufika asilimia 10 ifikapo 2025.”

Mkuu huyo wa nchi ametaja malengo mengine ni kuongeza mazao yanayouzwa nje kutoka Dola bilioni 1.2 hadi Dola bilioni 5, “ kama tutafuata mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo tunaweza kuvuka lengo hili.”
Malengo mengine kuongeza mashamba makubwa kutoka 110 hadi 1000, kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 665,000 hadi hekta milioni 1.2.

“Kwa malengo wizraa iliyojiwekea yakuongeza kilimo cha umwagiliaji kutoka asilimia 10 hadi asilimia 50 tunakwenda kuweka hekari milioni 18 kwenye umwagiliani.” amesema.

Amesema katika kuahakikisha malengo hayo yanatamia Serikali imeweka jitihada katika utafitikwa kuongeza bajeti kutoka Sh 7.35 hadi Sh 11 bilioni.

Amesema wamefanya hayo kwasababu “kilimo kinaweza kuivusha nchi na nimefanya kazi ya kilimo kama miaka tisa nikifanya kwenye mifugo na mazao.”

Ameongeza pia bajeti ya huduma za ughani “hiki kilikuwa kilio kikubwa” imeongezeka kutoka Sh 17.7 bilioni hadi Sh 51.45 bilioni.

Vilevile Serikali imeongoza uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora kutoka Sh 5.4 hadi Sh 10 .5 Bilioni na kuzipa fedha Wakala wa Chakula wa Taifa na Bodi ya MazaoMchanganyiko Sh 129 bilioni kwaajili yakununua na kuhifadhi mazao ya wakulima.

Ameongeza Serikali imekufungua masoko mapya ya mazao ikiwemo parachichi huko Uchina na Afrika Kusini, kupata maghala ya kukodi nje ya nchi tani 5000 Sudani Kusini na tani 2000 Lubumbashi nchini DRC na kwamba jitahada zingine zinaendelea kupata maghala China, Vietnam na Falme za Umoja wa Kiarabu.

“Tunafanya jitihada zote hizi ili wakulima wetu waweze kupata thamani ya jasho wanalolitoa, wale watu wa katikati wakwenda kununua mazao kwa bei ya chini wao wakauze bei ya juu hapana,” amesisitiza.

Kuhusu upotevu wa mazao baada ya uvunaji Rais Samia amesema wameelekeza kuanza kujenga maghala vijijini ambako ndiko wakulima walipo.

Takwimu zinaonyesha asilimia 30ya mzao yanayovunwa hupotea kutokana na kutokuwa na njia bora za uhifadhi.

Amesema katika hatua nyingine wameweza kufanikisha upatikanaji wa idhibati ya ubora kwaajili ya maabara yenye viwango vya kimataifa ya mamlaka ya mimea na viuatilifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!