Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mchezaji tenisi ashangaza ulimwengu kustaafu na miaka 25
Kimataifa

Mchezaji tenisi ashangaza ulimwengu kustaafu na miaka 25

Spread the love

 

MCHEZAJI namba moja Duniani katika mchezo wa tenisi, anayefahamika kwa jina la Asheleigh Barty, ameshangaza ulimwengu wa mchezo huo, kwa kutangaza kuwa atastaafu kucheza tenisi akiwa na umri wa miaka 25 pekee. Inaripoti BBC … (endelea).

Raia huyo wa Australia alitoa tangazo hilo, kwenye mitandao ya kijamii siku ya jumatano, akisema kuwa anaondoka ili kufuata ndoto zingine.

Amesema ‘’Nina furaha sana na niko tayari na ninajua kwasasa moyoni mwangu nina furaha ‘’ alisema kwenye video.

Hata hivyo, Barty alishinda Grand Slam yake ya kwanza kwenye French Open mwaka 2019.

Pia amebaki kuwa mchezaji wa nafasi ya juu tangu wakati huo, akiungwa mkono na mafanikio katika Wimbledon mwaka jana 2021.

Aidha mnamo Januari alikuwa mchezaji wa kwanza wa nyumbani, kushinda taji la Australia Open la wanaume na wanawake katika kipindi cha miaka 44.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!