May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DPP amwacha huru Abdul Nondo

Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania, Divisheni ya Iringa, imeifuta rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Iringa, wa kumuacha huru aliyekuwa Mwenyekiti Mtandao wa Wananfunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kesi hiyo imefutwa leo Jumatano, tarehe 23 Machi 2022, baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na rufaa hiyo.

Hati hiyo ya DPP imewasilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Basilius Namkambe, wakati rufaa ikienda kusikilizwa mahakamani hapo.

“Leo kesi ya Abdul Nondo ilipangwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa Iringa, mbele ya Jaji Lila, Kitusi na Mwampashi. Hata hivyo, Wakili Namkambe alisema DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, chini ya kanuni ya 77 (4) ya kanuni za Mahakama ya Rufaa. Mahakama imeondoa kesi hiyo,” imesema taarifa ya THRDC.

Sylivester Mwakitalu

Rufaa hiyo namna 30/2020, ilifunguliwa na DPP ikiwa ni takribani mwaka mmoja, tangu Nondo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, kuachwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Nondo alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili, ya kuchapisha taarifa za uongo kwa alitekwa nyara maeneo ya Ubungo, 2018 na kuzisambaza mtandaoni.

Huku shtaka lingie likiwa ni kutoa taarifa za uongo kwa Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mafinga, wilayani Mufindi,  Koplo Salim, kuwa alitekwa na watu wasiojuliakana na kupelekwa kiwanda cha Pareto Mafinga, mkoani Iringa.

Katika rufaa hiyo, Nondo atawakilishwa na Mawakili wa THRDC, ambao ni Jebra Kambole, Chance Luoga na Paul Kisabo.

error: Content is protected !!