Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Maneno ya mjane wa Magufuli kwa Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Maneno ya mjane wa Magufuli kwa Rais Samia

Spread the love

JANETH Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, amemheshimu kwa kukubali wito wake wa kushiriki hafla ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha mume wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Janeth ametoa kauli hiyo akitoa shukrani za Familia ya Hayati Magufuli, katika hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi, tarehe 17 Machi 2022, wilayani Chato, Geita, na kuhuduriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa dini.

Mjane huyo wa Magufuli, amesema Rais Samia alikubali kushiriki kumbukizi hiyo, licha ya kuwa na majukumu mengi ya kitaifa na kimataifa.

“Naomba nikiri kukupigia simu lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa, ila baadae ulivyonipigia nikakupa mualiko ambao uliupokea kwa moyo mkunjufu na ukaahidi kuja ingawa haikuwa kimaandishi,” amesema Janeth.

Janeth amesema “nashukuru kwa kuja licha ya kuwa una majukumu mengi umeniheshimu sana mama. Tunakuombea kwa Mungu akutie nguvu kuendelea kuliongoza Taifa vyema. Azidi kukujalia afya bora na maisha yako yazidi kuwa mema.”

Aidha, Janeth amewashukuru watu wote walioungana na familia yake, tangu alipofariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam, hadi leo inapoadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!