October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ya Rwanda yashutumiwa kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza

Spread the love

MAELFU ya Watu Wamenyanyaswa , kutishwa na kufunguliwa mashitaka kwa kuwa na maoni muhimu kuhusu Serikali ya Rwanda , Humani Raght Watch [HRW] inaeleza

Taarifa hiyo imetolewa makao makuu nchini Marekani leo alhamisi tarehe 17 machi 2022 imetaka kuachiliwa haraka kwa wanaharakati , waandishi wa Habari na Viongozi wa upinzani waliokamatwa nchini Rwanda .

Aidha mnamo mwaka 1994, hotuba za chuki zilitangazwa kwenye vyombo vya Habari , zilichangia kuchochea mauaji ya halaiki ya Rwanda ambayo yaliuwa watu takribani 800,000 ndani ya siku 100

Zaidi ya miaka miwili imepita , Human Right Watch imesema kuwa kukagua hotuba na kuwawekea vikwazo wanahabari , wanaotoa maoni yao Youtube kumepita kiasi .

Hata hivyo ripoti hiyo iliyoangaziwa na nyota wa Youtube anayefahamika kwa jina la Dieudonne Niyonsenga , imetazamwa mara milioni 15 lakini mtayarishaji huyo maudhui alishitakiwa na kutumikia kifungo cha miaka saba jera , kwa kosa la kuwadhalilisha maafisa wa Umma baada ya kuchapisha msururu wa video akiwashutumu Wanajeshi kwa kuwadhulumu watu wanaoishi katika vitongoji duni .

Serikali ya Rwanda inayoongozwa na Rais Paul Kagame haijatoa tamko lolote kuhusiana na ripoti iliyotolewa .

Shirika la Human Right Watch linatumaini ripoti yake italeta mwamko kuhusu ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza ulioripotiwa nchi .

error: Content is protected !!