Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari Chuo cha Mwalimu Nyerere chajivunia siku 365 za Rais Samia
Habari

Chuo cha Mwalimu Nyerere chajivunia siku 365 za Rais Samia

Spread the love

 

CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) nchini Tanzania kimesema, Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo aliyofanikiwa kuyafanya ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wake ni kuituliza nchi na kuchochea maendeleo ya Taifa na jamii kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais Samia Jumamosi hii ya tarehe 19 Machi 2022, atatimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani akichukua nafasi iliyoacha wazi na Rais John Magufuli ambaye alifariki dunia 17 Machi mwaka jana katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwaka mmoja wa utawala wa Rais Samia leo Alhamisi tarehe 17 Machi 2022 chuoni hapo Kivukoni, Mkuu wa MNMA, Profesa Shadrack Mwakalila alisema, ndani yam waka mmoja yamefanyika mengi katika kila sekta.

“Kipindi hiki tumeshuhudia utulivu, amani, tumeshuhudia furaha kwa Watanzania na hili linachochea hata maendeleo kwa sababu wananchi wanapokuwa katika hali ya utulivu na amani wanaweza kufanya majukumu yao vizuri,” amesema Profesa Mwakalila

Mkuu huyo wa chuo amesema, “katika maelekezo mbalimbali anayoyatoa kwa viongozi, watendaji na hata kwa jamii yote yanatusogeza karibu na yanarudisha kuwa wamoja kama Taifa jambo ambalo litamsaidia sana kupiga hatua kwenye maendeleo.”

Profesa Mwakalila amegusia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha mwkaa mmoja ni pamoja na kuboresha miundombinu katika Kampuni ya Kivukoni kwenye mabweni ya wanafunzi, madarasa na ofisi za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuweka umeme jua.

Amesema mchakato wa ujenzi wa maktaba kubwa na ya kisasa yenye uwezo wa kubebea wanafunzi 2,500 utaanza wakati wowote ukiwa na ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuingiza watu 1,000.

Profesa Mwakalila amesema, katika kampuni ya Karume Zanzibar kazi ya ujenzi wa mabweni yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,536 unaendelea vizuri na kwa mujibu wa mkataba ujenzi unatakiwa kukamilika 22 Desemba mwaka huu.

Amesema tawi la Pemba visiwani humo mshauri elekezi tayari ameshakamilisha kuandaa mpango kambabe wa eneo la chuo, usanifu wa majengo kwa ajili ya madarasa na mabweni na haya yote yamefanyika ndani ya kipindi cha mwkaa mmoja.

Amesema chuo kimetenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha wahadiri kufanya tafiti mbalimbali zenye maslahi kwa chuo na Taifa kwa ujumla na kuwa tayari wahadhiri wamejengewa uwezo wa kuandika maandiko ya utafiti na machapisho.

“Chuo kimewezesha wahadhiri 56 kwenda mafunzo kwa ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo shahada za uzamivu, uzamili na shahada ya awali na stashahada. Hivyo, idadi ya wahadhiri wenye shahada za uzamivu (PhD) imeongezeka hadi wahadhiri 40 waliopo chuoni,” amesema Profesa Mwakalila

Mkuu huyo wa chuo amesema, hadi kufikia Februari mwaka huu, chuo kimekuwa na bunifu nyingi na 22 zimeshindanishwa kwenye maonesho mbalimbali ambapo kati ya bunifu hizo moja ilishika nafasi ya pili kitaifa katika mashindano ya maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubinifu (MAKISATU) na nyingine ilishika nafasi ya nne Kitaifa katika maonesho yam waka 2020/21.

Aidha, Profesa Mwakalila amesema chuo kimefanikiwa kutoa mafunzo ya uongozi na maadili kwa viongozi na watendaji kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa chuo na kufanya idadi ya waliofuzu mafunzo hayo zaidi ya 4,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!