Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lema, Zitto hapatoshi, watupiana madongo
Habari za SiasaTangulizi

Lema, Zitto hapatoshi, watupiana madongo

Spread the love

WANASIASA wawili vijana na maarufu nchini, Godbless Lema na Zitto Kabwe wameingia kwenye vita nnzito ya maneno baada ya kila mmoja kuanza ‘kufukua makaburi ya mwenziwe’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Lema ambaye ni Mbunge wa zamani wa Arusha mjini (Chadema), kupitia kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Lema ameandika ujumbe ambao bila kumtaja mtu jina, unamuelezea kijana mmoja ambaye amefananisha na Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.

Lema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini ameandika: “Kuna Kijana mmoja ana-behave na anataka aonekane kama mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP lakini yeye akiwa mchangamfu zaidi.”

Aidha, muda mfupi baada ya kubandika ujumbe hu, Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi wa ACT Wazalendi na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TDC) aliibuka na kuujibu ujumbe huo chini yake.

Zitto ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kabla ya kuangushwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, akiandika: “Kijana huyo ndiye aliyekutoa wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa mwaka 2007. Kijana huyohuyo kwa kushiriakiana na wadau wakiwemo viongozi wako wa sasa ndiyo wataweka mazingira mazuri ya siasa. Endelea wailing sisi tunakuwekea mazingira mazuri ya kufanya siasa.”

Baada ya Zitto kujibu ujumbe huo, wachangiaji wengi wa mitandaoni walihusianisha majibizano hayo na kugundua kwamba kumbe aliyelengwa na Lema japokuwa hakuwa amemtaja jina, ni Zitto.

Zitto ni miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wapo katika kamati maalumu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kupitia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa siasa na vyama uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, mkutano ambao Chadema hawakushiriki.

Kutokana na maazimio ya mkutano huo, jana Rais Samia amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Dk. Pindi Chana, kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Hata hivyo, uamuzi huo umeonekana kupingwa na Lema ambaye amesema sheria zilizopo sasa ziendelee kutumika bila kutafutiwa kizuizi huku uboreshaji ukitafakariwa zaidi.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!