Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Rais Kenyatta amtangaza Odinga mrithi wake, aidhinishwa rasmi kuwania urais
Makala & Uchambuzi

Rais Kenyatta amtangaza Odinga mrithi wake, aidhinishwa rasmi kuwania urais

Spread the love

KIONGOZI wa Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga amepata ridhaa kuipeperusha bendera ya muungano wa Azimio la Umoja katika uchaguzi mkuu wa Kenya unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Agosti, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Raila Odinga aliidhinishwa kuwania urais katika kongamano kuu la Azimio la Umoja lililofanyika jijini Nairobi mapema jana tarehe 12 Machi, 2022.

Akiuhutubia mkutano huo wa kilele, Rais Uhuru Kenyatta alimshukuru kiongozi wa Wiper Democratic, Kalonzo Musyoka kwa kuunga mkono harakati za Raila Odinga na kusema kuwa,”hii ndio siku ambayo tunaianza safari itakayohitimishwa Agosti na itawaunganisha wakenya na nchi kwa jumla.”

Rais Kenyatta alikitaja kitendo cha Musyoka kuwa cha kishujaaa kwa ajili ya ushindi wa muungano wa Azimio.

Kongamano la Wajumbe 300

Rais Uhuru Kenyatta alilihutubia kongamano lililowaleta wajumbe zaidi ya 300 waliokusanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa KICC jijini Nairobi.

Rais Kenyatta alieleza kuwa ,”Mola ambariki Raila, rais wa tano wa Kenya kuiongoza Kenya. Nina imani kuwa Raila atalisogeza mbele taifa na kuhakikisha kuwa Kenya itaheshimika ulimwenguni.”

Kwa mtazamo huo wa Rais Kenyatta, Raila Odinga ana uwezo wa kupambana na ufisadi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pindi atakapokuwa rais ambaye hatamuacha yeyote nyuma.”Ninaamini hatawaacha ndugu zake nyuma.

Kwa sasa tumepata kiongozi wa kweli na serikali mpya itakapoundwa najua Raila atawasikiliza kiongozi wa Wiper Democratic Kalonzo Musyoka, Gideon Moi wa KANU, Gavana wa Kitui Charity Ngilu na wengine wengine”.

Vyama 26 kushirikiana na Azimio

Kiongozi wa Wiper Democratic, Kalonzo Musyoka aliutangaza msimamo wake rasmi na kumuunga mkono Raila Odinga wa Orange Democratic (ODM), kuwania urais.

Akiwa kwenye uwanja wa Jacaranda ulioko eneo la Embakasi jijini Nairobi alisema,” Niko tayari kumfanyia kampeni Raila Odinga…Raila Tosha.”

Hii ni mara ya tatu Kalonzo Musyoka kumuunga mkono Raila Odinga kuwania urais na ana imani kuwa anaweza kupambana na jinamizi la ufisadi linaloizonga Kenya.

Hotuba ya Raila

Kwenye hotuba yake baada ya kuipata ridhaa ya kuuwakilisha muungano wa Azimio la Umoja kwenye uchaguzi wa Agosti 9, Odinga aliahidi kuwa watadumisha umoja akiwa madarakani.

“Wakenya watafahamiana kama ndugu na marafiki,” amesema.

Kuhusu ushirikiano wake na kiongozi wa Wiper Democratic, Kalonzo Musyoka aliweka bayana kuwa,”Mimi na Kalonzo tulikuwa na tofauti kidogo ila tumezijadili na kufikia mwafaka. Tumeamua kushirikiana. Mimi sio kikaragosi cha Uhuru na wala yeye sio changu.” alisisitiza.

Kabla ya kufikia mwafaka huo, shughuli ya kumtangaza rasmi Raila Odinga kuwa mwakilishi wa Azimio la Umoja kwenye uchaguzi mkuu ilikumbwa na sintofahamu na kucheleweshwa.

Duru zinaeleza kuwa Kalonzo Musyoka wa Wiper Democratic alishikilia kuwa anataka apewe nafasi ya mgombea mwenza ambayo inaaminika kuwa imetengewa mwanasiasa atakayetokea eneo la Mlima Kenya lililo na wapiga kura wengi.

MAPAMBANO NA RUTO

Kwa mantiki hii, Raila Odinga atachuana na Naibu wa rais, William Ruto anayeupigia upatu muungano wa Kenya Kwanza.

William Ruto yuko kwenye msafara wa kampeni eneo la Mlima Kenya na tayari amepata ridhaa kuipeperusha bendera ya United Democratic Alliance (UDA) kwenye uchaguzi huo.

Muungano wa Kenya Kwanza unavileta pamoja vyama vikuu vya UDA, Ford-Kenya cha Moses Wetangula, Amani National Congress cha Musalia Mudavadi na vyengine vidogo.

Aidha, Muungano wa One Kenya Alliance (OKA), ukiongozwa na Gideon Moi (KANU), Martha Karua (NARC-Kenya) na Cyrus Jirongo (UDP) walitiliana saini makubaliano ya vyama 6 kushirikiana kisiasa siku ya Ijumaa tarehe 11 Machi, 2022.

Makubaliano hayo yalimhusisha pia Kalonzo Musyoka wa chama cha WIPER Democratic ambaye kwa sasa ametangaza waziwazi kumuunga mkono Raila Odinga kuwania urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja.

Uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika tarehe 9 mwezi wa Agosti mwaka huu.

Tayari tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imepata nahodha mpya Marjan Hussein Marjan ambaye amekuwa akikaimu nafasi hiyo tangu mwaka 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!