Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mrithi wa Angela Merkel apatikana Ujerumani
Kimataifa

Mrithi wa Angela Merkel apatikana Ujerumani

Olaf Scholz
Spread the love

MRITHI wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amepatikana leo mjini Berlin, kufuatia Bunge la nchi hiyo, kumuidhinisha Olaf Scholz kuwa Kansela mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Markel aliyeondoka madarakani, alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 16 na amekuwa Kansela wa kwanza mwanamke nchini Ujerumani.

Akitangaza matokeo hayo ya kura ya siri, Rais wa Bunge la Ujerumani, Bärbel Bas alisema, Scholz aliyekuwa naibu kansela na waziri wa fedha katika serikali ya muungano, ameidhinishwa kwa kura 395 katika Bunge lenye viti 736 kuchukua nafasi hiyo ya juu katika siasa za Ujerumani.

Vyama vitatu vya siasa, chama cha mrengo wa kushoto – Social Democrats (SPD), walinzi wa mazingira na waliberali, Free Democratic (FDP), ndio wamefunga mabaliano ya kuunda serikali.

Viongozi wa vyama hivyo, walikutana na kutia saini hati ya makubaliano yaliyofikiwa wiki kadhaa baada ya uchaguzi mkuu wa 26 Septemba.

Angela Merkel

Baada ya kuidhinishwa, Sholz na baraza lake la mawaziri lililo na wanachama 16, saba kutoka chama cha SPD watano kutoka chama cha kijani na wanne kutoka chama cha FDP, wanatarajiwa kuthibitishwa na rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kabla ya kuapishwa bungeni.

Baadaye mawaziri waliohudumu katika serikali ya Merkel pia watapewa nafasi hii leo kukabidhi madaraka kwa mawaziri wapya.

Scholz, aliyehudumu kama waziri wa fedha atamkabidhi majukumu hayo ya kifedha kiongozi wa FDP, Christian Lindner.

Serikali ya Scholz inaingia madarakani ikiwa na matumaini makubwa ya kuifanya Ujerumani kuwa ya kisasa zaidi kwa kukumbatia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi huku ikikumbwa na chamgamoto kubwa zaidi ya janga la corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!