May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia kuhutubia taifa leo

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

LEO Jumatano tarehe 8 Desemba 2021, saa 3:00 usiku, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atalihutubia taifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hii itakuwa hotuba yake ya kwanza kwa vyombo vya habari kuitoa, tangu aingie madarakani tarehe 19 Machi 2021, akichukua nafasi iliyoachwa na Rais John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia.

Rais Magufuli, alifariki dunia jioni ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Rais Samia atatoa hotuba hiyo ikiwa zimesalia saa chache, kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, uliopatikana 9 Desemba 1961 kutoka kwa Wakoloni.

Kilele cha sherehe hizo itakuwa kesho Alhamisi, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Rais Samia, atakuwa mgeni rasmi.

Channeli yetu ya mtandaoni ya MwanaHALISI TV itakuletea moja kwa moja hotuba hiyo huku mitandao yetu ya kijamii itakuwa ikiripoti hotuba hiyo.

MwanaHALISI TV itakuletea matangazo hayo moja kwa moja.

error: Content is protected !!