Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Miaka 60 ya Uhuru: Fataki kufyatuliwa maeneo matatu Dar leo
Habari Mchanganyiko

Miaka 60 ya Uhuru: Fataki kufyatuliwa maeneo matatu Dar leo

Spread the love

 

MILIPUKO salama ya fataki inalipuliwa leo Jumatano tarehe 8 Desemba 2021, kuanzia saa 5 usiku, katika maeneo ya Uwanja wa Taifa, Daraja la Kijazi (Ubungo) na Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kama sehemu ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kilele cha sherehe hizo ni kesho Alhamisi, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema, mlipuko hiyo itakuwa salama.

Ametoa onyo “kali na tahadhari katika kipindi hiki kuwa mtu yeyote atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu atashughulikiwa zaidi ya kawaida lakini kwa mujibu wa sheria za nchi.”

Kamanda huyo wa polisi, amewakumbusha wanaoendesha vyombo vya moto, kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuzuia ajali.

Aidha, Kamanda Muliro amesema, vikosi mbalimbali vya jeshi la polisi vikiwemo kikosi cha upelelezi, Field Force Unit (FFU), mbwa na farasi, polisi marine, Polisi Reli na Polisi Main Force (GD) vyote viko kazini lengo likiwa wananchi wote washerehekee maadhimisho ya miaka 60 ya UHURU wa Tanzania kwa amani bila hofu yeyote ile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!