Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama Kenya, yamkaanga Rais Kenyatta
Kimataifa

Mahakama Kenya, yamkaanga Rais Kenyatta

Spread the love
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameamrishwa kuwateua majaji sita waliosalia kati ya wale 40 , katika kipindi cha siku 14 zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Majaji hao sita wanashirikisha Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Ngugi, ambao walifaa kuhudumu katika mahakama ya rufaa.

Hakimu mkuu Evans Makori na msajili wa mahakama kuu Judith Omenge pia waliwachwa nje katika orodha ya majaji waliochapishwa katika gazeti la Kenya.

Siku ya Alhamisi , Jaji wa mahakama kuu William Musyoka , James Wakiaga na George Dulu walisema kwamba Jaji mkuu Martha Koome, pamoja na tume ya mahakama watakuwa huru kuwaapisha majaji hao sita iwapo Rais Uhuru Kenyatta atashindwa kutekeleza jukumu lake la kikatiba.

‘’Siku 14 zitakapokamilika, bila Uhuru kutangaza uteuzi huo, itabainika kwamba uwezo wake wa kuwateuwa utakuwa umekwisha na hivyobasi sita hao watakuwa wameteuliwa kama majaji wa mahakama ya rufaa kama ilivyopendekezwa’’, walisema majaji hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!