November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bocco mchezaji bora ligi kuu, Fei Toto shirikisho, Chama…

Spread the love

JOHN Raphael Bocco, Nahodha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, ametwaa tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa msimu 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Aidha, kiungo mahiri, Feisal Salum wa Yanga yeye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Shirikisho ‘Azam Sports Federation CUP’ (ASFC) msiku wa 2020/21 uliomalizika kwa Simba kutwaa ubingwa.

Wawili hao wametwaa tuzo hizo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizotolewa usiku wa Alhamisi, tarehe 21 Oktoba 2021, katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Aliyemkabidhi tuzo Bocco ni mgeni rasmi ambaye ni waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Bocco amewashinda Mukoko Tonombe wa Yanga na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Simba, Clotous Chama ambaye ametimkia Berkane ya Morocco.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Msimu uliopita, aliyetwaa tuzo hiyo alikuwa Chama.

Mbali na tuzo hiyo, Bocco ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kufunga magoli 16.

Pia, Chama ambaye ni raia wa Zambia, ametwaa tuzo ya kiungo bora wa ligi kuu, baada ya kuwashinda Mukoko Tunombe na Fei Toto wote wa Yanga.

Katika tuzo aliyotwaa Fei Toto, ni baada ya bameibuka mshindi kwa kuwashinda Louis Miquisson aliyekuwa Simba ambaye sasa amesajiliwa Al Ahly ya Misiri.

error: Content is protected !!