Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Michezo Twiga Stars yaichapa Zambia, yatinga fainali COSAFA
Michezo

Twiga Stars yaichapa Zambia, yatinga fainali COSAFA

Spread the love

 

TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imetinga fainali ya michuano ya COSAFA inayofanyika nchini Afrika Kusini. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo …  (endelea).

Ni baada ya kuwaondoa Zambia kwa mikwaju ya penati 3-2, leo Alhamisi, tarehe 7 Oktoba 2021.

Twiga na Zambia zilifika hatua ya kupigiana penati, baada ya kwenda sare ya 1-1 dakika 90.

Twiga walikuwa kwanza kupata bao dakika ya 17 kipindi cha kwanza kwa Zambia kujifunga. Zambia walirudisha goli hilo dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wao Chanda.

Katika mikwaju ya penati, mlinda mlango wa Twiga, Janeth Simba alipangua miwili kati ya tano zilizopigwa na kuwaondoa Zambia.

Nahodha wa Twiga, Amina Bilal amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Aidha, ikumbukwe tangu mashindano haya yaanze, Twiga wameruhusu bao moja katika mechi nne na hawajapoteza mchezo wowote ule katika michuano hiyo.

Hivyo, Twiga itasubiri mshindi kati ya wenyeji Afrika Kusini na Malawi watakaoumana katika fainali ya michuano hiyo ya COSAFA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

error: Content is protected !!