Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Halmashauri 21 zafikiwa na anuani za makazi
Habari Mchanganyiko

Halmashauri 21 zafikiwa na anuani za makazi

Spread the love

 

SERIKALI imesema jumla ya Halmashauri 21 tayari zimefikiwa na huduma ya Anuani za Makazi huku kazi ya kufikisha na kuunganisha nchi nzima na mfumo huo ikiendelea. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 7 Oktoba 2021 na Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA, Dk. Jim Yonazi wakati akifungua warsha kwa watoa huduma za posta nchini iliyofanyika Jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mtaa, nyumba, njia na barabara zinatambulishwa kwa anuani maalum chini ya utaratibu wa postikodi ili kurahisisha utambuzi na utoaji huduma za posta nchini.

“Serikali imejielekeza katika kuhakikisha tunakuwa na miundombinu rafiki katika usafirishaji na ugavi ndio maana serikali imewekeza fedha nyingi katika kuunda mfumo wa postikodi na anuani za makazi.

“Ningependa kuwashirikisha kwamba nchi nzima sasa ina postikodi zake” amesema.

Amebainisha kuwa mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) sasa utakuwa katika ukamilifu na kuwezesha utoaji huduma za posta na ufikishaji wa vifurushi na vipeto katika maeneo ya makazi, ofisi na sehemu za biashara.

Pia utasaidia utoaji wa huduma nyingine za jamii zikiwemo huduma za kutoa taarifa kwa zimamoto na polisi.

Aidha, amesema mfumo huo wa postikodi ulioanzishwa mwaka 2012, ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini.

Amesema kwamba kila kata ina msimbo wa tarakimu tano lengo ikiwa ni kuhakikisha kila barua au kipeto inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha au kifurushi kwa ajili ya urahisi wa kufikisha mzigo au barua husika panapostahili.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk. Jabiri Bakari amesema mamlaka hiyo imejidhatiti kuhakikisha huduma za posta nchini zinakuwa za ushindani kwa shabaha ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma badala ya kuachia huduma hizo kwa watumiaji wachache.

Amesema mamlaka hiyo tayari imetoa leseni za huduma za posta kwa watoa huduma 119 kote nchini ambao wanatoa huduma ya kusafirisha vipeto na mizigo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Haruni Lemanya amesisitiza umuhimu wa watoa huduma za posta hasa wanaosafirisha vifurushi na vipeto kuhakikisha wanatumia mbinu za kisasa na zenye weledi wakati wote wanapotoa huduma za posta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!