Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Diamond, Harmonize, Alikiba wachomoza tuzo Afrimma
Michezo

Diamond, Harmonize, Alikiba wachomoza tuzo Afrimma

Spread the love

 

WAANDAAJI wa tuzo za Afrimma (Afrian Music Magazine Awards) wametoa orodha mpya ya wasanii watakaowania tuzo hizo kwa mwaka 2021 huku Tanzania ikiwakilishwa na wasanii 10 wakiongozwa na Diamond Platnumz. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 19 na 21 Oktoba 19 mwaka huu, jijini Lagos nchini Nigeria huku dirisha la upigaji kura litafunguliwa rasmi Jumatatu tarehe 27 Septemba.

Afrimma imechagua nyimbo 400 kati ya nyimbo 8,880 zilizowasilishwa na wasanii.

Pia imeunda idadi ya wasanii 30 kutoka kwenye kanda 10 barani Afrika waliochaguliwa kuwania tuzo hizo.

Aidha, Tanzania imetoa wasanii 10 kati ya 30 wanaowania tuzo za Afrimma wakiongozwa na Diamond Platnumz ambaye ameingia kwenye vipengele sita.

Tanzania imetoa wasanii Harmonize, Alikiba, Nandy, Rosa ree, Rayvanny, Zuchu, Darassa, kwa upande wa mtayarishaji wa muziki na video wameingia Lizer classic kutoka WCB na Director Kenny wakati Dj bora Dj Sinyorita amechomoza katika kinyan’ganyiro hicho.

Na hivi ndio vipengele wanavyomwania wasanii kutoka Tanzania.

Msanii bora wa kike Afrika Mashariki – Nandy kupitia wimbo wake Nimekuzoea, Rosa ree – that girl na Zuchu kupitia wimbo wa Sukari.

Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, ameingia Darassa na wimbo wake wa “proud of you” aliomshirikisha Alikiba. Diamond Platnumz naye ameingia kupitia wimbo wa “Waah” aliomshirikisha Koffi Olomide.

Harmonize na wimbo wake “Atittude” aliomshirikisha Awilo longomba na H baba wakati Rayvanny kupitia wimbo wake wa Kelebe aliomshirikisha Inno’s b nao ametinga katika kinyang’anyiro hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!