May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uganda walegeza masharti ya Corona

Yoweri Museveni

Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni imetangaza kulegeza masharti dhidi ya janga la maambukizi ya Uviko-19 ambapo nyumba za ibada zitafunguliwa huku idadi ya watu watakaokuwa wakihudhuria sherehe mbalimbali hawatozidi 200. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Rais Museveni ametangaza kulegezwa kwa masharti hayo huku taifa hilo likiendeleza mapambano jitihada dhidi ya janga hilo hatari duniani.

Pamoja na masharti hayo kulegezwa lakini taasisi za elimu bado hazitafunguliwa huku Serikali ikitarajiwa kuwapa chanjo watu milioni 4.8 kabla ya shule na vyuo kufunguliwa.

Ifikapo tarehe 1 Novemba, 2021 vyuo na taasisi zingine za elimu ya juu zinatarajia kufunguliwa, lakini sekta ya elimu itafunguliwa rasmi Januari 2022.

Aidha, Rais Museveni amesema kuna dozi za chanjo ya Uviko-19 nchini humo milioni 2.2 na wastani wa dozi milioni 10 zaidi zinatarajiwa kuwasili miezi ijayo.

error: Content is protected !!