Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mapacha wazee duniani wavunja rekodi
Kimataifa

Mapacha wazee duniani wavunja rekodi

Spread the love

 

MAPACHA wawili raia wa Japan, Umeno na Koume wenye miaka 107, wamevunja rekodi ya kuwa pacha wazee zaidi duniani. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Kutokana na hilo, Umeno na Koume wameandikwakatika kitabu cha rekodi ya dunia ‘guinnes world record’ kama dada mapacha wanaofanana wakongwe duniani.

Kwa sasa, mapacha hao wana miaka 107 na siku 300 ambao walizaliwa tarehe 5 Novemba 1913 kwenye kisiwa cha Shodoshima, nchini Japan.

Awali, rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Kin na Gin, ambao walikuwa na miaka 107 na siku 175 hadi Kin alipofariki dunia Januari 2000.

Mwaka uliofuata yaani 2001, Gin alifariki dunia akiwa na miaka 108.

Mapacha hao, Kin na Gin ambao ssa ni marehemu, walizaliwa tarehe 1 Agosti 1892 huko Nagoya nchini Japan na walikuwa watu mashuhuri kwa vyombo vya habari katika kipindi cha muongo wao wa mwisho wa uhai.

Tuzo hizo zilitolewa jana Jumatatu tarehe 20 Septemba 2021, ambayo ilikuwa siku ya wazee duniani ambapo ni siku ya mapumziko ya kitaifa nchini mwao Japan.

Kutokana na ugonjwa wa korona (UVIKO-19) na tahadhari wadada hao mapacha wanaoishi sehemu tofauti za Japan walitumiwa vyeti vyao na wafanyakazi katika nyumba zao tofauti za utunzaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!