Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hatari! Cheki wanafunzi walivyojirusha ghorofani kumkimbia mshambuliaji, nane wamiminiwa risasi
Kimataifa

Hatari! Cheki wanafunzi walivyojirusha ghorofani kumkimbia mshambuliaji, nane wamiminiwa risasi

Spread the love

 

TAKRIBAN watu wanane wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya na mtu mwenye bunduki aliyefyatua risasi katika Chuo kikuu Perm kilichopo katika mji wa Perm nchini Urusi. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imesema, mshambuliaji huyo aliingia chuoni humo mapema leo tarehe 20 Septemba 2021 na kuanza kufyatua risasi hovyo.

Wanafunzi na walimu walijifungia ndani ya jengo la chuo hicho huku wengine walionekana wakiruka kutoka madirishani.

Haijulikani ni watu wangapi walijeruhiwa lakini polisi wa Urusi wamesema mshambuliaji huyo amekamatwa na kuzuiliwa.

Kamati hiyo inasema mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho kikuu.

Tukio hilo lilitokea katika chuoni hapo karibu kilomita 1,300 mashariki mwa mji mkuu, Moscow.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanafunzi wakirusha vitu vyao kutoka kwenye madirisha kwenye majengo ya chuo kikuu kabla ya kuruka kumtoroka mshambuliaji huyo.

Sehemu hii ya video ya wanafunzi wanaoruka nje ya madirisha ilitangazwa kwenye Runinga ya Urusi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!