TAKRIBAN watu wanane wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya na mtu mwenye bunduki aliyefyatua risasi katika Chuo kikuu Perm kilichopo katika mji wa Perm nchini Urusi. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).
Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imesema, mshambuliaji huyo aliingia chuoni humo mapema leo tarehe 20 Septemba 2021 na kuanza kufyatua risasi hovyo.
Wanafunzi na walimu walijifungia ndani ya jengo la chuo hicho huku wengine walionekana wakiruka kutoka madirishani.
Haijulikani ni watu wangapi walijeruhiwa lakini polisi wa Urusi wamesema mshambuliaji huyo amekamatwa na kuzuiliwa.
Kamati hiyo inasema mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho kikuu.
Tukio hilo lilitokea katika chuoni hapo karibu kilomita 1,300 mashariki mwa mji mkuu, Moscow.
Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanafunzi wakirusha vitu vyao kutoka kwenye madirisha kwenye majengo ya chuo kikuu kabla ya kuruka kumtoroka mshambuliaji huyo.
Sehemu hii ya video ya wanafunzi wanaoruka nje ya madirisha ilitangazwa kwenye Runinga ya Urusi.
Leave a comment