Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Daktari aua wanawe 2 kwa sumu, naye ajaribu kujiua
Kimataifa

Daktari aua wanawe 2 kwa sumu, naye ajaribu kujiua

Spread the love

 

DAKTARI mmoja mkazi wa Nakuru nchini Kenya anadaiwa kuwaua wanawe wawili kisha kujaribu kujitoa uhai usiku wa Jumamosi tarehe 18 Septemba mwaka huu. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Daktari huyo aliyefahamika kwa jina la James Gakara ambaye ni daktari wa uzazi katika hospitali ya Optimum Current Nakuru anadaiwa kuwadunga watoto wake wenye umri wa miaka 5 na 3 sindano yenye sumu na kufariki papo hapo.

Askari upelelezi walioitwa na majirani kuchunguza sababu za daktari huyo kujifungia ndani na watoto wake, jambo lisilo la kawaida, walikuta miili ya watoto hao ikiwa imelala kitandani huku povu likiwatoka midomoni.

Mshukiwa pia alikutwa akiwa amelala kitandani mwake akiwa na povu mdomoni ila hakuwa amekata roho.

Alikimbizwa katika hospitali ya Nakuru ambapo madaktari walinusuru maisha yake.

Dawa za zilizokutwa kwenye sirinji zilizokuwa zimetumika na kisu chenye makali ni baadhi ya vitu ambavyo vilipatikana kwenye eneo la tukio.

Kwa sasa mshukiwa anaendelea kupata nafuu hospitalini huku akisubiri kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la kikatili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!