Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Kibatala ahoji matumizi ya bisibisi, ajibiwa
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Kibatala ahoji matumizi ya bisibisi, ajibiwa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na wenzake wakiwa mahakamani
Spread the love

 

KIONGOZI wa jopo la mawakili wa utetezi katika shauri dogo la kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, Peter Kibatala, amehoji kama polisi aliyehusika katika ukamataji wa washtakiwa wawili katika kesi hiyo, anatoka Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Ugaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Inatokana na asili ya makosa wanayoshtakiwa ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wakili Kibatala amehoji hayo leo Jumatatu, tarehe 20 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Washtakiwa hao wawili waliokamatwa maeneo ya Rao mkoani Kilimanjaro Agosti 2020, kwa tuhuma za kujihusisha na kosa la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Akimhoji shahidi wa pili wa Jamhuri katika shauri hilo dogo, Inspekta Mahita Omari Mahita, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Wakili Kibatala alimuuliza kama kuna kikosi maalum kinachoshughulika na makosa ya ugaidi, ambaye alijibu hafahamu.

Wakili Kibatala alimhoji Inspekta Mahita, kama na yeye ni miongoni mwa wahusika wa kikosi hicho, ambaye alijibu akidai hapana.

Wakili Kibatala alimhoji swali hilo Inspekta Mahita, kwa kuwa alikuwa miongoni mwa Askari Polisi waliyoshiriki zoezi la kuwakamata watuhumiwa hao.

Mbali na kuhoji hayo, Wakili Kibatala alimtaka Inspekta Mahita, aieleze mahakama hiyo kama inaruhusiwa kutumia bisibisi kumtisha mtuhumiwa aliyekamatwa, ambaye alijibu akidai hairuhusiwi.

Pia, Kibatala alimhoji Inspekta Mahita akidai kama inaruhusiwa mtuhumiwa kufungwa pingu mikononi na miguuni sambamba na kupewa mateso hadi kushindwa kitembea, ambapo alijibu akidai hairuhusiwi.

Freeman Mbowe akiwasili mahakamani Kisutu

Wakili Kibatala alimhoji Inspekta Mahita akidai kama anafahamu mtuhumiwa wa pili, alifungwa machoni kwa kutumia jacketi lake jekundu, ambaye pia alijibu akidai hafahamu.

Shauri hilo lilitoka na mapinganizi ya Mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo na Kamanda Kingai, katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, katika mapingamizi hayo walihoji kwa nini mtuhumiwa alihojiwa Dar es Salaam, badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!