January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi akiwa Marekani

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Taarifa ya uteuzi imefanyika leo Jumatatu, tarehe 20 Septemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Rais Samia amefanya uteuzi huo akiwa ziarani nchini Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Walioteuliwa ni, Yona Killagane kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO).

Pia, amemteua Mathew Modest Kirama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Kabla ya uteuzi huu Kirama alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma (DE), Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kirama anachukua nafasi ya Nyakimura Mathias Muhoji ambaye amestaafu.

Uteuzi huo umeanza tarehe 18 Septemba, 2021.

error: Content is protected !!