Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Kaze afunguka kurejea Yanga
Michezo

Kaze afunguka kurejea Yanga

Spread the love

 

WAKATI fununu za aliyekuwa Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kwamba anarejea jangwani zikiendelea kushika kasi, kocha huyo amefunguka ujumbe mzito unaoashiria uamuzi alioufanya hivi karibuni. Anaripoti Mintanga Hunda, TURDACo … (endelea).

Kaze aliyehudumu Yanga kwa muda wa miezi mitano kama Kocha mkuu, safari hii anatajwa kuja kuwa Msaidizi wa Kocha wa Nesreddine Nabi.

Aidha, kufuatia mjadala huo Kaze ameandika hivi kupitia akaunti yake ya Facebook; “Wakati unaamua ni nani unayekutana naye maishani, moyo wako unaamua ni nani unayemtaka maishani mwako, na tabia yako ndio inayoamua nani abaki katika maisha yako.”

Kauli hiyo imewaibua mashabiki wa Yanga akiwamo Willson Anfield ambaye alijibu hivi; “Yanga bado tunakuhitaji kutokana na ushirikiano wako hata baada ya kuondoka kwani ulionyesha una mapenzi na hii klabu.

Naye Tumaini Mhanjilwa akaongeza hivi; “Karibu tena nyumbani tunaimani na wewe na pia wewe ni milele…”

Tarehe 7 Machi mwaka Yanga ilitangaza kuachana na Kaze aliyekuwa amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili kuanzia tarehe 16 Oktoba, 2020.

Pia msaidizi wake Nizar Halfan, kocha wa makipa Vladimir Niyonkuru na ofisa usalama wa klabu, Mussa Mahundinao pia walitimuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!