August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga warejea kimyakimya

Spread the love

 

KLABU ya Yanga imerejea nchini usiku wa kuamkia leo ikitokea Nigeria ilikokwenda kupepetana na River United ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kombe la klabu bingwa Afrika. Anaripoti Mintanga Hunda TUDARCo … (endelea).

Yanga imerejea huku ikiwa imepoteza mchezo wake huo wa jana na kutupwa nje ya mashindano hayo ya kimataifa.

Ikumbukwe kwenye mchezo wa awali uliochezwa Dar es salaam Yanga ilifungwa bao 1-0 na kutolewa nje ya mashindano kwa jumla ya idadi ya magoli 2-0.

Uongozi wa klabu hiyo umetoa malalamiko mbalimbali juu ya vitendo walivyofanyiwa na uongozi wa Rivers United pamoja na kucheleweshewa majibu ya vipimo vya Covid 19 ambayo pia yalionesha wachezaji kadhaa wa Yanga wanamaambukizi.

Baada ya kurejea, Yanga sasa wanajipanga kupepetana na watani wao wa jadi – Simba kwenye mchezo wa ngao ya jamii ambao utafanyika tarehe 25 Septemba 2021 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

error: Content is protected !!