TARATIBU za mazishi ya Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia, Dk. Kenneth David Kaunda zimeanza rasmi leo Jumatano, tarehe 23 Julai 2021 na zitahitimishwa 7 Julai 2021. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Dk. Kaunda alifariki dunia tarehe 17 Juni 2021, katika moja ya hospitali iliyopo Lusaka nchini Zambia, akiwa na miaka 97.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na rais wa sasa wa taifa hilo, Edgar Lungu, mwili wa Dk. Kaunda utapitishwa katika majimbo 10 ya taifa hilo, ili kutoa fursa kwa wananchi kumuaga.
“Ni matakwa ya familia ya Kaunda, kwamba mwili wake upelekwe kwenye majimbo yote 10 ili wananchi wapate fursa ya kumuaga mpendwa wao.”
“Wakati tunaendelea na maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, baba wa taifa hili, Dk Kenneth David Kaunda, serikali yangu, kwa kushauriana na familia ya Kaunda, imeweka utaratibu mzuri. Ziara hizo zitaanza Jumatano, Juni 23 na zitahitimishwa tarehe 5 Julai 2021.”
“Katika mazishi haya, lazima nisisitize kwamba taratibu zote zitafanywa kwa kuzingatia tahadhari ya na sheria zote za kupambana na Covid-19 kama inavyoelezwa na Wizara ya Afya,” amesema Lungu.
Rais Lungu amesema, kuaga kitaifa kutafanyika tarehe 2 Julai 2021, ambapo viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya taifa hilo watahudhuria.
“Mwishowe, rais wetu mwanzilishi wa taifa hili atazikwa katika makaburi ya viongozi huko Lusaka mnamo tarehe 7 Julai. Ninawahimiza raia wote kushirikiana na mamlaka wakati taratibu za mazishi zikiendelea.
Dk. Kaunda alikuwa ni mmoja wa kundi la mwisho la wapigania uhuru barani Afrika. Alitawala Zambia kwa miaka 27 kuanzia tarehe 24 Oktoba 1964 hadi 2 Novemba 1991.
Leave a comment