SERIKALI ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), imeeleza, hakuna mgonjwa yeyote wa corona visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Mansor Mazrui, Waziri wa Afya wa Zanzibar jana tarehe 22 Juni 2021, katika mahojiano na Kituo cha Utangazaji cha Uingereza (BBC).
“Nikuthibitishie kwamba Zanzibar hatuna mgonjwa hata mmoja wa corona, wodi zetu zipo wazi. Sisi bado hatupimi corona hapa kwa wageni wanaaoingia nchini, tunapima wakati wa kutoka nchini.”
“Kwa sababu wakati wa kutoka wanahitajia mashirika ya ndege ili wakiondoka waoneshe certificate (vyeti) zao, lakini wanaokuja nchini hapa wanakuja na certificate zao. Kwa hiyo watu wote wanaokuja hapa wanakuja na certificate zao zinazoonesha negative (hawana).”
Mazrui amesema, kutokana na utaratibu wa wa wageni kuingia viswani humo nav yeti vyao vinavyoonesha hawana virusi hivyo, Zanzibar mpaka sasa haina rekodi yoyote ya maambukizi hayo.
Amesema, “kwa hiyo, mpaka sasa hatuna mgonjwa hata mmoja wa COVD-19 Zanzibar, si raia si mzanzibari yeyote kutoka nje, bado hatujapokea kesi hiyo.”
Tanzania ambapo Zanzibar ni sehemu yake, imewatangazia wananchi wake kuchukua tahadhari zaidi kuhusu wimbi la tatu la virusi vya corona.
Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya maeneo ya mkusanyiko tayari yametoa tahadhari na ulazima wa kuvaa barako, miongoni mwayo ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Leave a comment