Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tuhuma za rushwa: Mwenyekiti CCM akwepa jela, alipa faini
Habari Mchanganyiko

Tuhuma za rushwa: Mwenyekiti CCM akwepa jela, alipa faini

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Maisaka mkoani Manyara, Bakari Yangu, amekwepa kifungo cha miaka miwili gerezani, kwa kulipa faini ya Sh. 300,000, baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kuomba rushwa, iliyokuwa inamkabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Katika kesi hiyo Na. CC.24/2020, Bakari alidaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 200,000, kutoka kwa Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Komoto mkoani humo, Daniel Tango, ili amuachie kiwanja kilichokuwa mali ya CCM.

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 28 Mei 2021 na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), mkoani Manyara, Holle Makungu.

Taarifa ya Makungu imesema kuwa, baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobero, kutoa hukumu hiyo jana tarehe 27 Mei 2021, Bakari alilipa faini hiyo na kukwepa kwenda jela.

“Baada ya kukiri makosa yake, mahakama ilitoa adhabu hiyo, ambapo mshtakiwa Bakari aliweza kulipa Sh. 300,000 na hivyo kukwepa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela,” imesema taarifa ya Makungu.

Ikielezea mchakato wa kesi hiyo, taarifa ya Makungu imesema, hukumu hiyo ilitolewa baada ya mshtakiwa huyo kukiri makosa yake.

“Bakari amehukumiwa baada ya kukiri makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mwinjilisti Tango, kinyume cha kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya 2007, ili wamwachie mwinjilisti huyo kiwanja ambcho mwenyekiti huyo alidai ni mali ya CCM,” imesema taarifa ya Makungu.

Kesi hiyo Na. CC.24/2020, ilifikishwa mahamani hapo na mawakili wa Takukuru, Martin Makani, akisaidiwa na Evelyne Onditi, tarehe 26 Juni 2020.

Awali, Bakari alikana makosa yake, lakini baada ya Takukuru kuwasilisha mahakamani hapo vilelezo na ushahidi uliomtia hatiani, aliamua kukiri makosa yake.

“Baada ya kukana makosa yake, mawakili waliwasilisha vilelezo na ushahidi ulioiwezesha mhakama kumuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu, baada ya kutakiwa kujitetea, aliamua kutoisumbua mahakama kwa kukiri makosa yae yote ya kuomba na kupokea rushwa kama alivyoshtakiwa,” imesema taarifa ya Mkaungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!