Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kigogo Bandari aliyetoroka, apandishwa kizimbani kwa utakatishaji fedha
Habari Mchanganyiko

Kigogo Bandari aliyetoroka, apandishwa kizimbani kwa utakatishaji fedha

Pingu
Spread the love

 

ALIYEKUWA Mhasibu katika Bandari ya Kigoma, Madaraka Robert Madaraka, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, kwa tuhuma za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), mkoani Kigoma, Stephen Mafipa, Madaraka amepandishwa kizimbani leo tarehe 28 Mei 2021.

Madaraka anadaiwa kuisababisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), hasara ya Sh. 619,278,260.

“Takukuru kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tunamfikisha mahakamani aliyekuwa Mhasibu Bandari ya Kigoma, kwa tuhuma za ufujaji na ubadhirifu, kuisababisha TPA hasara ya Sh. 619,278,260.52 pamoja na utakatishaji fedha,” amesema taarifa ya Mafipa.

Taarifa ya Mafipa imesema kuwa, Madaraka ambaye awali alitoroka, ataunganishwa na washtakiwa wengine wanne, katika Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 5/2020, linaloendelea mahakamani hapo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Eliya Stephano Ntinyako, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ntinyako Company Limited. Morris Charles Mchindiuza, aliyekuwa Meneja wa Bandari Kigoma. Herman Ndiboto Shimbe, aliyekuwa Afisa Uhasibu TPA Kigoma na Lusubilo Anosisye Mwakyusa, aliyekuwa Afisa Rasilimali watu TPA Kigoma.

“Uchunguzi wa Takukuru Makao Makuu ulibaini kwamba, mtuhumiwa huyu alitoroka kabla ya ofisi yetu kuanza uchunguzi Februari 2020.

“Hivyo basi, tunapenda kuuarifu umma kuwa, ofisi yetu iliendelea kumtafuta mtuhumiwa huyu hadi ilipofanikiwa kumpata na hivi leo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili,” imesema taarifa ya Mafipa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mafipa, Madaraka anatuhumiwa kuongoza genge la kufanya ubadhirifu wa fedha, katika kituo cha Bandari ya Kigoma, wakati akiwa mhasibu katika kituo hicho.

Mbali na kufikishwa kizimbani, taarifa ya Mafipa imesema Takukuru inaendelea na uchunguzi wa tuhuma nyingine zinazomkabili Madaraka.

“Sambamba na kumuunganisha Madaraka katika shauri hili, uchunguzi wa TAKUKURU Makao Makuu bado unaendelea kufanyika dhidi yake, kwa tuhuma zingine za uhujumu uchumi na kuisababishia hasara TPA,” imesema taarifa ya Mafipa na kuongeza:

“Mara baada ya uchunguzi huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake pamoja wengine walioshirikiana naye.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!