Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari Samia aonya uhalifu Dar, ampa maagizo IGP Sirro
HabariHabari MchanganyikoTangulizi

Samia aonya uhalifu Dar, ampa maagizo IGP Sirro

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo (IGP), Simon Sirro, akomeshe vitendo vya uhalifu katika Mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Ijumaa, tarehe 7 Mei 2021, katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam, akizungumza na wazee wa mkoa huo.

Kiongozi huyo wa Tanzania, ametoa agizo hilo akisema, ameona taarifa za ongezeko la vitendo vya uhalifu katika mitandao ya kijamii.

“Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kwamba Dar es Salaam wanajaribu kina cha maji. Ujambazi na upokonyaji umeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP Sirro uko hapa, naomba ushughulikie,” amesema Rais Samia.

 

Sambamba na hilo, Rais Samia amesema, baadhi ya wananchi mkoani humo wanashauri kiongozi wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam abadilishwe, aletwe mwingine na kumuagiza IGP Sirro asuhughulikie ushauri huo.

“Na katika mitandao ile wananchi wanasema alikuwuepo afande nani (hakumtaja jina), alikuwepo hapa wakasme mama turudishie, naomba hilo uliangalie vizuri,” amesema Rais Samia.

Kwa sasa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inaongozwa na Lazaro Mambosasa, aliyeteuliwa na IGP Sirro Agosti 2017.

Mambosasa aliteuliwa kurithi mikona ya IGP Sirro, baada ya kamanda huyo kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli, kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!