July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ATCL yazindua safari Dar- Guangzhou

Spread the love

 

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), limezindua safari za moja kwa moja za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou, nchini China. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uzinduzi huo umefanywaa leo Jumamosi, tarehe 8 Mei 2021 na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamliho, katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi mbalimbali wa ATCL wamehudhulia uzinduzi huo wa ndege itakayokuwa ikitumia saa 11, akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Mhandisi Matindi amesema, safari hizo zitakuwa kila siku ya Jumamosi na kurudi Jumapili na zitakuwa kila baada ya wiki mbili.

error: Content is protected !!