Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Bilioni 7.15 kutatua tatizo la madawati shule za msingi
Elimu

Bilioni 7.15 kutatua tatizo la madawati shule za msingi

Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati darasani
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetenga Sh.7.15 bilioni, kwa ajili ya kutengeneza madawati 710,000 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yatakayotumika shule za msingi. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka.

“Je, serikali imechukua hatua gani kukabiliana na upungufu wa walimu na madawati hasa baada ya elimu ya msingi na sekondari kuwa bure,” alihoji Mwakasaka.

Akijibu swali hilo, Silinde alisema, Serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi katika kutatua changamoto ya madawati kwenye shule za msingi na secondari nchini.

Alisema, ili kukabiliana na upungufu wa madawati katika mwaka wa fedha 2021/2022 serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza madawati.

“Serikali imeendelea kuajiri walimu wa shule za msingi na sekondari ambapo kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 walimu 33,684 na mafundi sanifu maabara 497 wameajiriwa,” alisema Silinde

Alisema, “Ofisi ya Rais-Tamisemi, kwa kushirikiana na ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri walimu 6,000 ifikapo 30 June 2021, ikiwa ni ahadi ya utekelezaji wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!