Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndege tatu mpya kutua nchini
Habari za Siasa

Ndege tatu mpya kutua nchini

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
Spread the love

 

NDEGE tatu zitatua nchini muda wowote baada ya Serikali ya Tanzania, kukamilisha malipo ya ununuzi wa ndege hizo tatu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Katika ndege hizo tatu, mbili ni Airbus A220-300 na moja ni Dash 8-Q400De-Havilland. Ndege hizo zinatarajiwa kuwasili kati ya 2021 na 2022.

Kuwasili kwa ndege hizo, kutafanya jumla ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa jumla ya ndege  12.

Kauli ya ununuzi wa ndege hizo imetolewa leo tarehe 13 Aprili 2021, bungeni mjini Dodoma na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wakati akiwasilisha mwelekezo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/22.

“Nitumie fursa hii kulipongeza Shirika la Ndege Tanzania    kwa    kuanzisha safari za kwenda Guangzhou, China,” amesema Waziri Majaliwa.

1 Comment

  • Hao wasafiri wa Guangzu ni kina nani? Watanzania wanaruhusiwa kuingia huko bila ya chanjo na barakoa? Au watasema wao wanalindwa na kupendelewa na Mungu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!