May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kero Jangwani, Dar kumalizwa hivi

Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani

Spread the love

 

KERO ya kujaa maji eneo la Jangwani, Dar es Salaam ambapo husababisha adha kubwa ya usafiri kwa wananchi, ipo mbioni ‘kutibiwa.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Serikali imesema, ipo katika mchakato wa kujenga tuta kubwa katika eneo hilo ili kuondoa kabisa kero hiyo iliyotesa wananchi kwa muda mrefu pale mvua zinaponyesha.

Kauli hiyo imetolewa na David Silinde, Naibu Waziri wa Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), leo Jumanne tarehe 13 Aprili 2021, bungeni mjini Dodoma.

Silinde alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Agnes Kaiza aliyehoji, ni lini serikali itamaliza kero ya wananchi wa Dar es Salaam hasa eneo la Jangwani?

“Serikali imeweka mkakati wa kumaliza kero hiyo kwa kujenga miundombinu itakayopitisha maji ili yasituame na kuwa kero,” amesema.

Amesema, serikali inatengeneza mkakati maalumu wa kuhakikisha inajenga miundombinu imara ya kuondoa matatizo hayo.

error: Content is protected !!