NDEGE tatu zitatua nchini muda wowote baada ya Serikali ya Tanzania, kukamilisha malipo ya ununuzi wa ndege hizo tatu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Katika ndege hizo tatu, mbili ni Airbus A220-300 na moja ni Dash 8-Q400De-Havilland. Ndege hizo zinatarajiwa kuwasili kati ya 2021 na 2022.
Kuwasili kwa ndege hizo, kutafanya jumla ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa jumla ya ndege 12.
Kauli ya ununuzi wa ndege hizo imetolewa leo tarehe 13 Aprili 2021, bungeni mjini Dodoma na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wakati akiwasilisha mwelekezo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/22.
“Nitumie fursa hii kulipongeza Shirika la Ndege Tanzania kwa kuanzisha safari za kwenda Guangzhou, China,” amesema Waziri Majaliwa.
Hao wasafiri wa Guangzu ni kina nani? Watanzania wanaruhusiwa kuingia huko bila ya chanjo na barakoa? Au watasema wao wanalindwa na kupendelewa na Mungu?